Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linatarajia kupokea wakuu wa nchi kuanzi August 16, 2019 ambapo ulinzi utaimarishwa kuanzia mapokezi yao Airport, Hoteli wanazofikia na kuelekea katika kumbi za mikutano.
Taarifa ya Jeshi hilo imeeleza kuwa wataimarisha ulinzi na vikosi vyote vya doria mbwa, farasi na helicopter ili kuhakikisha mkutano unamalizika salama.
Sambamba na hilo wanaendelea Kukamata pikipiki zote na magari yanayovunja sheria na katazo la kuingia mjini ambapo jumla ya magari na pikipiki ni 126 ambayo yamechukuliwa hatua za kisheria.
"Madereva wengi wameendelea kutupa ushirikiano katika siku zote za mkutano huu wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara SADC," imeeleza taarifa hiyo.
Tuesday, August 13, 2019
Magari na Pikipiki 126 zakamatwa kwa kuingia Mjini Dar
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment