Na Ahmad Mmow, Lindi.
Msafara wa viongozi wa chama cha ACT- Wazalendo wa mkoa wa Lindi umeporwa gari na watu wanatajwa kuwa ni walinzi wa chama cha CUF.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Lindi, mwenyekiti wa mkoa wa Lindi wa chama hicho, Isihaka Mchinjita alisema msafara wa viongozi wa nne wa mkoa wa Lindi ukiwa katika kijiji cha Nachunyu, wilaya ya Lindi umeporwa gari na watu waliotajwa kuwa ni walinzi wa CUF-Chama Cha Wananchi.
Mchinjita alisema viongozi hao wakiwa katika kijiji hicho kwenye kikao na wanachama wa
viongozi wa CUF. Ambao baadhi yao walikiri kuwa unyang'anyi huo ulitekelezwa kutokana na maagizo yao, kwamadai kwamba gari hiyo ni yao ( mali ya chama cha CUF),'' alisema Mchinjita.
Hata hivyo mwenyekiti huyo alilitupia lawama jeshi la polisi, hasa kituo cha Lindi kwakushindwa kuzuia gari hiyo kuondoka na wanyang'anyi hao kutoka mkoani Lindi.
Kiongozi huyo alisema baada ya kutokea tukio hilo walitoa taarifa kituo cha polisi cha Lindi wakiwa na kadi ya gari iliyoporwa. Ambapo polisi iliwasiliana na mamlaka ya mapato (TRA) na kujiridhisha kwamba ni mali ya Nassoro Mazrui.
'' Polisi ilitoa amri gari hiyo ipelekwe katika kituo hicho. Hata hivyo haikupelekwa, na hali wakijua gari hiyo itatoroshwa lakini hawakuchukua hatua kuzuia isitoroshwe kwa madai kwamba hakuna unyang'anyi. Bali gari hiyo inagombaniwa kutokana na mgao wa mali za CUF. Walisema hawafungui jalada,'' aliongeza kusema Mchinjita.
Alipoulizwa kamanda wa polisi (RPC) wa mkoa wa Lindi, Pudensiana Protas alikiri kwamba tukio hilo limetaarifiwa kwa jeshi hilo.
Huku akiweka wazi kwamba uchunguzi umeanza na unaendelea.
Juhudi za kuwapata viongozi wa CUF ili kupata maelezo yao kuhusu sakata hili jipya zinaendelea
kwakasi kubwa ili kusikia maelezo ya pande zote ili kukidhi matakwa matakwa ya sheria na maadili ya uandishi wa habari.


No comments:
Post a Comment