China imetishia kulipiza kisasi iwapo Marekani itaendelea na mpango wake wa kuongeza ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini Marekani zinazogharimu dola bilioni 300.
Wizara ya fedha ya China imesema itachukua hatua inayohitajika kukabiliana na viwango vipya vya ushuru.
Hatua ya Marekani kuongeza ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za China zinazogharimu dola bilioni 300, inakiuka makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda na yanayoinukia kiuchumi, G20, katika mkutano wao wa kilele uliofanyika nchini Argentina na Japan mwaka mmoja uliyopita.
Ujumbe wa wafanyabiashara wa China wanatarajiwa kusafiri kuelekea Marekani mwezi ujao kujadili suala hilo.
Hapo jana Rais Donald Trump wa Marekani alichukuwa muelekeo mpya katika mazungumzo hayo akipendekeza kuwa anaweza kukutana na Rais Xi Jinping wa China kuzungumzia suala la mgogoro wa kisiasa unaoendelea Hong Kong.
Thursday, August 15, 2019
China yatishia kulipiza kisasi kwa Marekani
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment