Waziri wa Madini, Doto Biteko amefuta leseni elfu kumi na mbili kati ya elfu thelasini na tatu kwenye machimbo ya Tanzanite Mirerani zilizo kutwa na makosa mbali mbali ikiwemo kushindwa kutekeleza wajibu wao.
Biteko amesema wameamua kuvifutia usajili kwa sababu ya kukiuka sheria za uchimbaji ikiwemo kutolipa kodi huku akisema kuwa hatowafumbia macho wale wote wanaojipa haki wasiyo stahili.
Waziri Biteko amechukua hatua hiyo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi katika mji mdogo wa Mirerani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara yanapochimbwa madini ya Tanzanite.
Mbali na hayo Wizara ya Madini imekabidhiwa ripoti ya kamati teule ya wizara hiyo kwa kushirikiana na wajumbe kutoka mkoa wa Manyara iliyokuwa ikichunguza mgogoro kati ya wachimbaji wadogo wa kitalu B na D pamoja na kampuni ya tanzanite one kitalu C.
Akiwasilisha ripoti hiyo mbele ya Waziri wa Madini katika mji mdogo wa Mererani mwenyekiti wa kamati hiyo Hamisi Kamando amesema kuwa kufuatia ripoti waliyoiwasilisha wanaomba serikali itatue tatizo la mipaka ya vitalu hivyo ili kuwepo na mahusiano mazuri.
Akizungumza mara baada ya kupokea ripoti hiyo Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuwa ripoti hiyo ameipokea na wizara yake itaifanyia kazi mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha mgogoro wa vitalu hivyo unapatiwa ufumbuzi.
Ameongeza kuwa wachimbaji wa madini na wafanyabiashara wanapaswa kufuata taratibu za kupata leseni za uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi kwani wasipofuata sheria hizo watafutiwa leseni zao za uchimbaji.
Naye Naibu wa Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka wafanyabaishara wa madini kuacha tabia ya utoroshaji wa madini kwani kufanya hivyo hukwamisha maendeleo ya wananchi wanyonge wasio na hatia huku akisema kuwa serikali haitawahurumia wale wote watakao husika na vitendo hivyo vya kuhujumu rasilimali za Taifa.
Monday, July 29, 2019
Wizara ya Madini yavifutia leseni Vitalu elfu 33 Machimbo ya Tanzanite
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment