Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya julai ,18,2019 walifanikiwa kukamata meno ya Tembo 05 yakiwa yanasafirishwa kwanjia ya pikipiki yenye uzito wa kg 24.55 na dhamani ya shilingi 170,000,000.
Kamanda mkoa wa kipolisi,Tarime na Rorya,Henry Mwaibambe leo ameaambia waandishi wa habari Ofisini kwake kuwa julai,18,2019 majira ya saa5.50 usiku katika barabara itokayo kijiji cha Kubiterere kwenda kijiji cha Ng’ereng’ere Askari polisi wakiwa katika msako pamoja na Task Force Taifa walifanikiwa kuwakamata Mseti Daniel 27 mkazi wa kijiji cha Nyabitocho na Peter Maina 25 mkazi wa kijiji cha Ng’ereng’ere wakiwa na meno ta Tembo matano.
Kamanda Mwaibambe aliongeza kuwa wameyahifadhi men ohayo katika mfuko wa Sandarusi na walikuwa wanasafirisha kwa kutumia usafiri wa Pikipiki yenye namba za usajili MCBQ aina ya Sanlg.
“Meno hayo yanauzito wa kilogramu 24.55na yanadhamani ya shilingi milioni miamoja sabini na laki saba(170,000,000) watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani tarehe 26,julai,2019 na shauri la uhujumu uchumi kuandikishwa 40/2019”alisema Mwaibambe.
Jeshi hilo limetoa wito kwa jamii kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano ili kuwasema wahalifu ambapo amewataka wale wote ambao wanatafuta kipato kwanjia isiyo halali kuacha tabia hiyo mara moja kwani mkono wa sheria hautawaacha salama pindi wanapopatikana wakifanya biashara hiyo.
Kwa upande wake Mrakibu mwandamizi wa polisi Geoger Katangazi ambaye pia ni RCO Tarime na Rorya alisema kuwa jamii inatakiwa kuacha kujihusisha na biashara haramu ambazo zinawasababishia hasara na kupoteza mda mwingi wa kufanyabiashara halali.
Katangazi aliongeza kuwa jeshi la polisi lina mkono mrefu na ushirikiano kwa hali hiyo wahalifu wanatakiwa kuacha tabia ya uhalifu kwani hapapo watakapokimbilia hata kama ni nchi jirani ya Kenya jeshi hilo linaushirikiano mzuri litawasaka hadi kuwakamata wahalifu.
Monday, July 29, 2019
Polisi wakamata meno ya tembo yenye dhamani ya shilingi milioni 17
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment