Adbox

Tuesday, July 16, 2019

Wabunge wanne washutumu matamshi ya Trump

Rais wa Marekani Donald Trump akikaidi shutuma kali kuhusu matamshi yake ya kibaguzi, ameendeleza madai yake kwa wabunge wanne wanawake wa chama cha Democrat wenye asili ya kigeni kuondoka nchini humo mara moja, akikoleza mzozo huo ambao umesaidia kumuingiza katika Ikulu ya Marekani ya White House na kudai watu wengi wanamuunga mkono.

Wabunge hao wanne walimshambulia Trump, wakimshutumu kwa kile walichokiita matamshi ya chuki dhidi ya wageni, na kurudia miito kwa wabunge wa Democrats kuanza mchakato wa kumshitaki bungeni.

Trump amewataka wabunge hao wanne kurejea makwao walikotoka katika nchi zao ambazo zimeharibika zilizojaa uhalifu katika maandishi yake katika ukurasa wa Twitter matamshi ambayo kwa kiasi kikubwa yameshutumiwa kuwa ni ya kibaguzi.

No comments:

Post a Comment

Adbox