Adbox

Saturday, July 6, 2019

Tutankhamun: Kwanini Misri inataka mnada kwa kichwa cha mfalme usitishwe?


Tutankhamun bustHaki miliki ya picha
Image captionSerikali ya Misri inataka mnada usitishwe
Misri imetoa agizo kwa umba la kupiga mnada Christies kusitisha uuzaji wa mchongo wa kichwa cha mfalme mdogo Tutankhamun wenye umri wa miaka 3,000.
Wizara ya mambo ya nje Misri inatuhumu kwamba mchngo huo huenda uliibiwa katika miaka ya 1970 kutoka hekalu moja.
Mchongo huo wa inchi 11 ulitarajiwa kupigwa mnada leo London na unatarajiwa kugharimu zaidi ya $ milioni 5.
Christies inasema Misri haijaelezea wasiwasi kuhusu kichwa hicho katika siku za nyuma licha ya mchongo huo 'kuonyeshwa wazi'.
Mchongo huo uliotengenezwa kwa jiwe gumu la madini ya quartz linatoka katika mkusanyiko binfasi wa sanaa ya jadi ambalo jumba hilo la mnada la Christie liliuza kwa pauni milioni 3 mnamo 2016.
Katika taarifa yake, Christies imesema: "Mchongo huo hauchunguzwi na haujawahi kuchunguzwa."
Imesema haiwezi kupiga mnada kitu ambacho kinagubikwa na malalamiko ya halali.
Christies pia imechapisha mpangilio wa wamiliki wa mchongo huo katika miaka 50 iliyopita.

Tutankhamun ni nani?

  • Tutankhamun alifariki zaidi ya miaka 3000 iliyopita akiwa na umri wa miaka 19.
  • Masalio ya mwili wake yaligunduliwa mamo 1922.
  • Alikuwa farao katika enzi iliyojulikana kama Ufalme mpya katika historia ya Misri.
  • Tangu kugunduliwa kwa kaburi lake, amefahamika kama Mfalme Tut.
  • Jina lake halisi, Tutankhamun, lina maana "Picha halisi ya Amun".
  • Ugunduaji wa kaburi lake ulishinikiza hamasa kutoka kwa umma kutaka kufahamu zaidi kuhusu hitoria ya Misri.
  • Mnamo Februari 2010, utafiti wa jeni au DNA ulithibitisha kuwa alikuwa mtoto wa maiti iliyokaushwa katika kaburi la KV55, linaloaminika na baadhi kuwa ni la Akhenaten.
Inafahamika kwamba mchongo wa kichwa chake mfalme Tut kilipatikana kwa Mjerumani mwenye hadhi Prinz Wilhelm von Thurn kati ya 1973 na 1974.
Jumba la mnada la Christies limeongeza kwamba uwepo wa mchongo huo wa kichwa umejulikana kwa muda mrefu sasa na ulionyeshwa hadharani kwa miaka kadhaa.
Waziri wa zamani aliyehusika na vito vya thamani kutoka Misri Zahi Hawass ameliambia shirika la habari la AFP: "Tunadhani mchongo huo uliondoka Misri baada ya 1970 kwasababu katika wakati huo vito vingine muhimu viliibiwa kutoka hekalu la Karnak."
Misri iliidhinisha sheria mnamo 1983 kupiga marufuku kuondoshwa kwa vito kutoka nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Adbox