Frank Lampard amepigwa picha katika uwanja wa Stamford Bridge anapokaribia kuwa kocha mpya wa Chelsea. (Mail)
Kuidhinishwa kwa Lampard kuwa kocha mpya wa Chelsea kulicheleweshwa Jumatano jioni baada ya mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram kukumbwa na changamoto za kiufundi hali ambayo ilifanya kuwa vigumu kuchapisha picha au kuweka video mtandaoni. Klabu hiyo ilitaka mitandao hiyo ya kijamii kurejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kufanya tangazo hilo. (Mirror)
- Wachezaji wapya waliojiunga na ligi ya Uingereza
- Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 03.07.2019
- Nani kuvaana na nani 16 bora Afcon?
Chelsea pia imeanza mazungumzo ya kandarasi mpya ya na kiungo wa kati wa miaka 20 Mason Mount, amabaye aliichezea Derby msimu uliopita chini ya ukufunzi wa Lampard. (Evening Standard)
Manchester United wanataka kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24 kutoka Sporting Lisbon. (Sky Sports)
Tottenham imesitisha mazungumzo yake na Real Betis kumhusu kiungo ya kati wa Argentina Giovani Lo Celso, 24, baada ya vilabu kushindwa kuafikiana malipo. (Sky Sports)
Arsenal wamepewa nafasi ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mbrazil Malcom, 22, lakini azma yao kubwa ni kumnasa mshambuliaji wa Ivory Cost wa miaka 26, Wilfred Zaha kutoka Crystal Palace. (Mirror)
Gunners wana pauni milioni 70 wanapojianda kuweka dau la pili la kumnunua Zaha, japo kuwa Palace wanamini thamani ya mshambuliji huyo ni pauni milioni 80(Sky Sports)
Manchester City huenda wakamsaini mlinzi wa Uholanzi wa miaka 24 Nathan Ake kutoka Bournemouth msimu huu. (L'Equipe - in French)
Tottenham wanamtaka mashambulizi wa roma na timu ya taifa ya Italia Nicolo Zaniolo, 22, na wako tayari kumuuza mlinzi wa Ubeliji Toby Alderweireld, 30, ili wapate fedha za kugharamia mkataba huo. (Mail)
Agenti wa Romelu Lukaku amaefanya mazungumza mapya na Inter Milan lakini klabu hiyo ya Italia bado inashauriana na Manchester United kuhusu ada ya kiungo huyo wa Ubelgiji aliye na miaka 26. (Sky Sport Italia - in Italian)
Bayern Munich wameipiku Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaini beki mkabaji wa Ureno Joao Cancelo,25, kutoka Juventus. (Corriere dello Sport via Manchester Evening News)
Everton wamepokea maombi kutoka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Ujerumani maarufu Bundesliga na hampionship ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa miaka 22, Joe Williams. ((Liverpool Echo))
Southampton hawana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Ureno Andre Silva, 23, kutoka AC Milan licha ya tetesi kutoka Italia kuashiria vingine. (Daily Echo)
Tottenham huenda ikawauza beki wa England Kieran Trippier, 28, na Danny Rose, 29, wanapojianda kutoa maombi ya kumnunua mlizi wa Fulham muingereza Ryan Sessegnon, 19.(Mirror)
Newcastle imewasiliana na kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez okuhusu uwezekano wake kuchukua nafasi ilioachwa wazi na Rafael Benitez kama meneja wao mpyaa. (Sun)
Tetesi Bora Jumatano
Atletico Madrid wanataka kumsajili Alexandre Lacazette kuchukua nafasi ya mshambuliaji Antoine Griezmann, 28 ambaye anaelekea Barcelona. (Mirror)
United watalazimika kilipa zaidi ya pauni milioni £90 kumnunua beki wa Leicester City na England, Harry Maguire - hatua itakayomfanya kuwa nyota huyo wa miaka 26 kuwa mlinzi ghali zaidi . (Telegraph)
Barcelona wako tayari kupokea maombi ya kumnunua mlinzi wa kati wa miaka 25-Mfaransa Samuel Umtiti, ambaye analengwa na Manchester United. (Sport, via Mirror)
Real Madrid wana mpango wa kumjumuisha mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, katika mkataba utakaowawezesha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mail)
Winga wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, hana mpango wa kuondoka Nou Camp msimu huu wa joto licha ya vilabu vikubwa Ulaya ikiwa ni pamoja na Liverpool na Bayern Munich kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (L'Equipe)
Chelsea wameafikiana kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu na kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 23. (Telegraph)
Mlizi wa Arsenal Mfaransa Laurent Koscielny, 33,ananyatiwa na Bordeaux. (L'Equipe)
No comments:
Post a Comment