Adbox

Thursday, July 4, 2019

App za Facebook, Instagram, WhatsApp zashindwa kupakia na kupakua picha

Nembo ya Facebook kwenye smartphoneHaki miliki ya picha
Baadhi ya watumiaji wa Facebook, Instagram na WhatsApp walishindwa kuweka picha, video na mafaili.
Facebook, inayomiliki App zote tatu, imesema inafahamu kuhusu tatizo hilo na ilikuwa ''ikifanyia kazi ili kurudisha kila kitu sawa haraka iwezekanavyo''.
Mitandao ya kijamii, ina mabilioni ya watumiaji wake ulimwenguni.
Washindani wake Twitter pia walikuwa na tatizo kwa watumiaji wake kushindwa kutuma ujumbe wa moja kwa moja au kupokea taarifa kuhusu ujumbe ulioingia.
Kampuni iliomba radhi kwa dosari hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakisema kuwa wanashughulikia tatizo hilo.
Watumiaji bado waliweza kuweka ujumbe kwenye twitter na ujumbe wa hashtag #instagramdown ukaanza kushika kasi mtandaoni wengi wakitumia kueleza matatizo ya mshindani wake.
App ya Facebook Messenger, ambayo huwa inapakuliwa kivyake, nayo ailiathirika.
Mwezi Machi, Facebook na Instagram ilipata changamoto za kiteknolojia ambayo ilidumu wa muda. Matatizo pia yalikumba app zote mbili sambamba na Whats App mwezi Aprili.
Facebook ina watumiaji zaidi ya bilioni 2.3 kwa mwezi wanaotumia app hiyo na Instagram ina watumiaji bilioni moja.

No comments:

Post a Comment

Adbox