Rais John Magufuli amewataka polisi kufanyakazi na kuvipongeza vikosi vyote vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa palipo na amani ndipo maendeleo yanapoweza kupatikana.
Ameyasema hayo wakiti akizindua rasmi nyumba 15 za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo Mkoani Geita ambazo zitakuwa na uwezo wa kutumiwa na Askari 30.
"Watanzania tuitunze amani, wazee tuitunze amani, makabila tuitunze amani, Tanzania hii ni tajiri sana kila kitu kipo, inawezekana siku za baadaye hata hapa tulipo wanaweza kuanza kuchimba polepole..." Rais John Magufuli.
Amgomea IGP Sirro kambi hiyo kuitwa jina lake na kuagiza liitwe jina lake ili aweze kusimamia vema ujenzi huo na kuongeza kuwa iwapo hautakamilika aibu hiyo impate yeye mwenyewe
Monday, July 15, 2019
Tanzania hii ni tajiri sana kila kitu kipo - Rais Magufuli
Tags
# Habari
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Habari
Tags:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment