Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) imejipanga kutumia fursa ya maonyesho ya Nane nane iyakayofanyika kitaifa mkoani Simiyu kutangaza fursa za wananchi kutalii katika hifadhi ya Serengeti .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akizungumza na Wanahabari katika makao makuu ya Tanapa amesema kuwa maonyesho hayo yanalenga kuhamasisha utalii wa ndani na kupata watanzania watakaopata fursa ya kutembelea hifadhi ya Serengeti kwa gharama nafuu .
Aidha amesema kuwa maonyesho hayo yatafunguliwa na makamu wa Raisi Samia Suluhu na kufungwa na Raisi John Pombe Magufuli huku Viongozi na watu mashuhuri wakitarajiwa kushiriki.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Maendeleo ya biashara katika hifadhi ya Serengeti Milliam mwakilema amesema kuwa kwa kipindi cha siku za maonyesho kutakua na magari yatakayowapeleka hifadhini kwa bei ya punguzo.
"Tunatoa ofa Maalumu Safari za kwenda Serengeti kila siku zitakua zikifanyika kuanzia tarehe 4 mpaka 11 saa kumi na mbili asubuhi ,gharama ni za kawaida kwa mtu mzima atalipa sh 30,000 na mtoto atalipa sh 10,000" Alisema Mwakilema

No comments:
Post a Comment