Adbox

Thursday, July 18, 2019

Rais Magufuli alikumbuka jambo la mwaka 1973

Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Mwaka 1973 Baba wa Taifa Mwl Nyerere aliamua Makao Makuu ya nchi yawe Dodoma.

Rais Magufuli amesema kuwa mwaka huo yeye alikuwa darasa la Sita huku akisema tangu yuko huko hadi leo ndoto ya Baba wa Taifa ilikuwa haijatimia.

''Mwaka 1973 Baba wa Taifa Mwl Nyerere aliamua Makao Makuu ya nchi yawe Dodoma. Mimi nilikuwa shule ya msingi darasa la Sita, kwahiyo toka mimi niko huko hadi namaliza Elimu yangu, ndoto ya Baba wa Taifa ilikuwa bado haijatimia, nafurahi sasa imekamilika,'' Rais Magufuli ameyasema leo Dodoma wakati akzingumza na wananchi wa Kongwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox