Adbox

Saturday, July 27, 2019

Raia wa Uturuki waliotekwa Nigeria waokolewa

Raia 4 wa Uturuki waliotekwa nyara na watu wasiojulikana nchini Nigeria waachiwa huru.

Raia hao 4 wa Uturuki, Yasin Çolak (33), Şener Paşa (40), Ergün Yurdakul (35) na Seyit Emre Çelik (25) walitekwa nyara na watu wasiojulikana wiki iliyopita kilomita 500 kutoka  mji mkuu wa Abuja katika jimbo la Kwara. Oparesheni illiyofanywa kwa ushirikiano wa askari polisi na askari jeshi ilifanikisha raia hao kupatikana wakiwa salama salmini.

Raia hao wa Uturuki walipelekwa katika ubalozi wa Uturuki mjini Abuja wakiwa na afya njema

No comments:

Post a Comment

Adbox