Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amewataka wananchi pamoja na Wadau wengine welevu kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo hususan katika masuala ya maendeleo ambapo kwa kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Shinyanga, wameweza kujenga nyumba kumi zenye vyumba vitatu vitatu kila moja.
IGP Sirro amesema hayo wakati akiwa mkoani Shinyanga, kwa ziara ya kikazi na kupata fursa ya kutembelea mradi huo wa Ujenzi wa nyumba za makazi ya askari ambapo amewaomba wananchi kuendele kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Polisi nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainabu Telack, amewataka askari watakaoishi kwenye nyumba hizo kuendelea kuzitunza ili kuzidi kuziongezea thamani.
Mhe. Talack amesema kuwa, ni vyema jitihada zilizofanywa na Rais Dkt. John Magufuli, zikaendelea kuungwa mkono na wadau mbalimbali ili kuhakikisha askari Polisi wanakuwa na makazi bora ya kisasa.
No comments:
Post a Comment