Adbox

Friday, July 12, 2019

Mahakama inayotembea yazinduliwa Mwanza

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imezindua mahakama inayotembea (Mobile Court) ambayo itatoa huduma katika maeneo ya Buswelu, Igoma na Buhongwa ikiwa ni mpango mkakati wa Mahakama Kuu nchini kupunguza changamoto za msongamano wa mashauri mahakamani sanjari na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Akizindua Mahakama hiyo, Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda hiyo ya Mwanza, Sam Rumanyika ambaye alitangulia kwa kutoa Salamu za rambirambi kwa Kampuni ya Azam Media kufuatia msiba wa wafanyakazi wake watano na madereva wawili amesema Mahakama hiyo ni ya kisasa na ya pili nchini na itakayorahisisha utoaji wa huduma na haki kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Adbox