Mahamakama ya kisutu nchini Tanzania imemuachilia huru mlimbwende Wema Sepetu lakini ikamkamata tena dakika chache baadaye alipokuwa akiondoka mahakamani humo.
Kufikia sasa haijabainika ni kwa nini msanii huyo wa filamu alikjamatwa tena.
Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, Malkia huyo wa urembo wa mwaka 2006 anakabiliwa na mashtaka ya kurekodi video ya ngono na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.
Mwishoni mwezi Juni 2019 mahakama hiyo ilikuwa imemuonya msanii huyo wa filamu kutokiuka masharti ya dhamana la sivyo itaifutilia mbali dhamana yake.
- Tamasha la Nicki Minaj lazua gumzo Saudia
- Hasira Misri kuhusu kupigwa mnada kichwa cha mfalme
- Korea Kaskazini yaikosoa Marekani kwa kuendeleza 'uhasama'
Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania kauli hiyo ilitolewa na hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo Maira Kasonde wakati alipokuwa akitoa uamuzi kuhusiana na masharti ya dhamana.
Mnamo tarehe 17 mwezi Juni mwaka huu mahakama hiyo iliamuru bi Wema apelakwe Rumande hadi juni 24 baada ya mshtakiwa kujisalimisha katika mahakama hiyo baada ya kutoa hati ya kukamatwa kwake kufuatia hatua yake ya kutowasili mahakamani bila ya kutoa taarifa.
Wakili wa Wema, Ruben Simwanza alieleza kuwa mteja wake alikuwemo mahakamani, lakini aliugua na akalazimika kuondoka - ufafanuzi ambao haukuiridhisha mahakama.
"Kama amekuja mahakamani halafu akaondoka bila kutoa taarifa, mahakama itajuaje kama alikuja? Alishindwa nini kutoa taarifa mahakamani", alisema hakimu.
Wema amewahi kushtakiwa katika kesi nyingine kwenye mahakama hiyo ya Kisutu mnamo 2017 kwa mashtaka ya umiliki wa mihadarati.
Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 4 mwezi Februari 2017, Wema na wenzake walipatikana wakimiliki misokoto ya bangi katika eneo la Kunduchi Ununio.
Mahakama ilimpata na hatia Juali 2018 na kumpiga faini ya shilingi milioni mbili za Kitanzania.
Maafisa wa polisi nchini Tanzania walianzisha msako dhidi ya watu maarufu baada ya baadhi yao kuhusishwa na ulanguzi wa mihadarati
No comments:
Post a Comment