Misri kwa mara ya kwanza imeyafungua mapiramidi ya kale tangu mwaka 1965. Waziri wa Mambo ya Kale Khaled el-Anany amewaeleza waandishi wa habari kuwa watalii sasa watapata nafasi ya kuingia katika mapiramidi ya Bent na mengine ya karibu, ambayo yapo umbali wa karibu kilomita 40 kusini mwa mji mkuu, Cairo.
Mapiramidi hayo ya Bent yaliyo na urefu wa mita 79, yalijengwa kwa nasaba ya nne ya mwanzilishi wa Farao, karibu miaka 2,600 kabla ya Kristo.
Yanachukuliwa kuwa na upekee kwa ajili ya vyumba vyake viwili vya ndani. Wanaakiolojia pia waligundua mkusanyiko wa mawe, udongo na mbao baadhi yake zikiwa na mabaki ya miili ya binadamu pamoja na mabaki ya ukuta wa kale.
Serikali nchini Misri inajaribu kufufua sekta ya utalii ambayo iliyumba kufuatia wimbi la vuguvugu la mapinduzi la mwaka 2011 lililomuondoa madarakani Hosni Mubarak.
Sunday, July 14, 2019
Misri kwa mara ya kwanza yafungua mapiramidi ya kale
Tags
# Habari
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Habari
Tags:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment