Adbox

Tuesday, July 16, 2019

Mh. Rais ni aibu mno na sisi ni wanyonge katika masuala ya usafiri - Askari Magereza

Askari Magereza katika Gereza la Butimba wamuomba Rais Magufuli vitendea kazi yakiwemo magari.

Askari hao wamesema hawana magari na wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa kuwabeba mahabusu na wafungwa katika magari mabovu sanjari na mkuu wa gereza kutokuwa na gari linaloweza kumsaidia katika kazi zake za utendaji.

" Mheshimiwa Rais ni aibu mno na sisi ni wanyonge katika masuala ya usafiri, tena Tanzania nzima, tunaomba utusaidie kutupatia magari ikibidi coastal na makazi yetu hayako katika hali nzuri." Mmoja wa askari Magereza

Baada ya maombi hayo, Rais Magufuli naye akajibu, "Kwa maaskari Magereza nimesikia kilio chenu ninyi hamna tofauti na majeshi mengine na hamuwezi mkawa mnafanya kazi kwa kulalamika, hakikisheni hawa wafungwa hawaingii na simu gerezani, nyembe, wanaofanya biashara na hawa wafungwa wasifanye.” .

No comments:

Post a Comment

Adbox