Adbox

Sunday, July 28, 2019

Maiti ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa China kuchomwa kesho

Maiti ya aliyekuwa waziri mkuu wa China, Li Peng itachomwa kesho katika mji wa Beijing.

Li, ambaye alifariki Julai 22 akiwa na umri wa miaka 91 alihudumu kama mwanachama wa bunge la 12 la chama cha kikomunisti cha China (CPC), mwanachama wa kamati kuu ya CPC, mwenyekiti wa kamati ya bunge miongoni mwa nyadhifa zingine.

Bendera ya taifa itapeperushwa nusu mlingoti katika bustani ya Tian'anmen Square, afisi zote za CPC, maeneo ya Hong Kong, Macao na afisi zingine za serikali kwa heshima ya kiongozi huyo

No comments:

Post a Comment

Adbox