Iran imewakamata na kuwahukumu adhabu ya kifo majasusi wa CIA
Iran inadai kuwa imewakamata majasusi 17 ambao inasema wamekuwa wakifanyia kazi shirika la ujasusi la Marekani CIA, na kuwahukumu kifo baadhi yao.
Wizara ya Intelijensia imesema kuwa washukiwa hao wamekuwa wakikusanya taarifa kuhusu mpango wa nyuklia, jeshi na sekta zingine nchini humo.
Rais wa Marekani Donald Trump, amepuuzilia mbali madai hayo akisema kuwa ni ''uwongo mtupu".
- Mzee Mwinyi akerwa na January Makamba
- Ronaldo hana kesi ya kujibu
- Mtembo: Mti wa usuluhisho huko Mwika Tanzania
Washington na Tehran zimekuwa zikizozana kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na hali ya taharuki imekuwa ikiongezeka kati ya mataifa hayo mawili.
Mwaka jana Bw. Trump aliiondoa Marekani katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia wa Iran na kuliwekea upya vikwazo vya kiuchumi taifa hilo.
Katika wiki za hivi karibuni mataifa hayo yalikaribia kukabiliana kijeshi katikaeneo la Ghuba.
Akizungumza muda mfupi baada ya tangazo lililotolewa na Iran kuhusu kukamatwa kwa maafisa hao, Trump alisema: " inakuwa vigumu kwangu kufikia mkataba na Iran."
Tunafahamu nini kuhusu 'kesi ya ujasusi'?
Iran inasema kuwa majasusi wanaoaminiwa kufanyia kazi Marekani wamekamatwa katika kipindi cha miezi 12 hasi mwezi Marchi mwaka huu.
Watu hao 17, wote ni raia wa Iran wanaofanya kazi katika "vituo maalum" vya kijeshi, mitambo ya nyuklia na sekta ya kibinafsi na wamekuwa wakifanya kazi mmoja mmoja, alisema afisa wa Iran wa ujasusi anayeshikilia cheo ja juu amewaambia wanahabari.
Hakusema ni wangapi waliohukumiwa kuuawa na ikiwa hukumu dhidi yao tayari imetekelezwa.
"Hukumu ya watu hawa imetolewa, na baadhi yao wamehukumiwa kifo kama 'wafisadi duniani' [Kosa ambalo adhabu yake chini ya sheria ya Kiislam inayotekelezwa nchini Iran]," Mkuu wa kitengo cha ujasusi amenukuliwa na shirika la habari la wanafunzi nchini Iran(ISNA).
Siku ya Jumapili, Waziri wa intelijensia wa Mahmoud Alavi alitangaza kuwa taarifa ya kina kuhusu kukamatwa kwa majasusi hao wanaohusishwa na Marekani itaoneshwa katika Televisheni ya Kitaifa ya Iran.
Wizara ya Intelijensia ya Iran pia ametoa kanda ya video inayoonesha kionjo cha taarifa hiyo maalum, inayoangazia jinsi majasusi hao walivyokutana na pia kuwahojooi maafisa wa serikali akiwemo Bw. Alavi.
Baadhi ya majasusi hao walianguka katika ''mtego wa visa" uliyowekwa na CIA kwa raia wa Iran wanaotaka kusafiri nchini Marekani, Bw. Alavia aliongeza kuwa : "Wengine walifikiwa wakati walipokuwa wakiomba visa, huku wengine waliokuwa na visa kuanzia mwanzo wakishurutishwa na CIA kuomba wabadilishiwe upya hati hiyo muhimu ya usafiri ."
Wengine walihadaiwa kuwa watapata hela nyingi pamoja na kazi za hadhi ya juu na kutoa huduma za matibabu, alisema.
Televisheni ya Kitaifa ya Iran imetangaza makala maalum kuhusu kuvunjwa kwa ''mtandao wa CIA ".
Mwezi uliopita, Iran ilisema kuwa imefanikiwa kuvunja mtandao unaohusishwa na CIA, lakini haikuwa wazi ikiwa tangazo hilo lilikuwa na uhusiano na kisa hicho .
Kuna mvutano wa madaraka Iran?
Uchambuzi wa mmwandishi wa BBC Kasra Naji, BBC
Wadadisi wengi wa siasa za Iran wanatilia shaka madai ya hivi punde yanayotolewa na mamlaka ya nchi hiyo.
Siku ya Jumatatu wizara ya Intelijensia ilisema kuwa imevunja mtandao wa wa majasusi wanaoshirikiana na shirika la ujasusi la Marekani CIA, mwizi uliopita.
Lakini ikajikanganya na kuongeza kuwa watu 17 wanaoshukiwa kuwa majasusi wa Marekani walikamatwa mwaka jana.
Baadhi yao wanaamini idadi kamili ya waliokamatwa ni 17 kwa kushukiwa kuwa majasusi kwa miaka mingi na wote ni Wairan.
Kwa mujibu wa nyaraka kutoka jela la Evin, kuna wafungwa wengi wanaozuiliwa hapo kwa tuhuma za kuwa majasusi wa mataifa tofauti.
Lakini kwa nini Wizara ya Intelijensia imekuja na taarifa hii sasa ni kuwa huenda ni kutokana na uhasama kati yake na kitengo cha intelijensia cha Jeshi la Iran.
Wiki mbili zilizopita Runinga ya kitaifa ya Iran ilitangaza makala ya iliyoimiminia sifa kitengo hicho cha intelijensia na kuonesha serikali ya rais Hassan Rouhani kama isiyokuwa na uwezo wowote mbele ya ujasusi wa mataifa ya magharibi.
Na sasa, Wizara ya intelijensia inajibu makala hiyo kwa kuangazia ufanisi wake katika suala la kukabiliana na ujasusi
Uhasama uliopo kati ya mashirika ya kintelijasia ni ishara wazi kuwa kuna mvutano wa madaraka unaoendelea hadharani na kila mmoja anajionea hilo kupitia runinga ya kitaifa.
Mvutano wa sasa umesababishwa na nini?
Hali ya taharuki kati ya Iran, Marekani na Uingereza inaendelea kushuhudiwa kufuatia msururu wa visa vya utekaji meli za mafuta katika eneo la Hormuz:
- Ijumaa iliopita Iran ilikamata meli ya mafuta iliyokuwa na bendera ya Uingereza katika maji yake. Tehraniliwahi kuonya kuwa italipiza kisasi hatua ya Uingereza kukamata meli yake ya mafuta katika pwani ya Gibraltar mapema mwezi huu.
- Wiki iliopita Bw. Trump alisema kuwa jeshi la majini la Marekani limeharibu ndege ya Iran isiyokuwa na rubani baada ya kukaidi maagizo lakini Iran inapinga madai hayo.
- Mwezi uliopita, Iran ilidungua ndege ya upelelezi ya Marekani isiyokuwa na rubani iliyokuwa ikipaa katika anga lake, na kuilaumu kwa kukiuka sheria ya anga lake. Lakini majeshi ya jeshi la Marekani linasema ndege hiyo ilikuwa ikipaaa katika anga ya kimataifa, na kulaani vikali hatua ya Iran kuwa ya uchokozi.
- Marekani pia iliilaumu Iran kwa kushambulia mara mbili meli za mafuta katika Ghuba ya Oman mwezi Mei na Juni - tuhuma ambazo Tehran imekana.
Hali ya taharuki kati ya mataifa hayo mawili imeongezeka siku za hivi karibuni tangu Marekani ilipoiwekea Iran vikwazo vipya vinavyolenga sekta yake ya mafuta baada ya kujiondoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment