Baadhi ya waandamanaji waliingia kwa nguvu
kwenye jengo la bunge la Hong Kong, wakitishia
kuvuruga shughuli za serikali.
kwenye jengo la bunge la Hong Kong, wakitishia
kuvuruga shughuli za serikali.
Waandamanaji Hong Kong wamevamia bunge la
nchi hiyo katika maadhimisho ya leo ya mji huo
kurejeshwa katika utawala wa China mwaka wa
1997, wakati kukiwa na hasira ya umma kuhusiana
na sheria ambazo zitaruhusu watuhumiwa kupelekwa
China bara kufunguliwa mashitaka.
Maandamano hayo yamekuwa ni hatua ya moja kwa
moja ya kuipinga serikali ya China kuwa na mkono
wake katika uendeshwaji wa mji huo wenye mamlaka
ya ndani. Baadhi ya waandamanaji waliingia kwa nguvu
kwenye jengo hilo, wakitishia kuvuruga shughuli za
serikali lakini haikufahamika mara moja ni wangapi
walibaki ndani.
Maelfu ya wanaharakati wa kidemokrasia walifanya
maandamano mengine ya amani leo mchana, wakimkata
kiongozi wa mji huo anayeegemea serikali ya China
kujiuzulu na kubatilisha kile wanachokiona kuwa ni
miaka mingi ya kushuka kiwango cha uhuru.
No comments:
Post a Comment