Adbox

Saturday, March 14, 2020

Waziri Biteko akasirishwa na Mkataba wa Mchuchuma na Liganga

Na Ezekiel Mtonyole


Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema umefika wakati kuachana na mkataba wa kinyonyaji wa uchimbaji wa madini ya chuma cha Liganga na makaa ya mawe ya mchuchuma uliopo wilayani Ludewa mkoani Njombe ambao hadi sasa umechukuwaa muda mrefu bila faida yoyote kwa serikali na wananchi.

Waziri Dotto Biteko ambaye  yupo mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi amesema moja ya vitu ambavyo vinachelewesha ni kung’ang’ania mikataba ambao unafunga fursa kwa wananchi.

 ‘’Kuna watanzania ambao wanaweza kufanya kazi na wakazalisha chuma,wakatengeneza na choka niliwaona mwenyewe kwenye maonyesho,chuma hapa hapa wakatengeneza wenyewe,watu wazuri kabisa alafu awawezi kupata matilio eti kwa sababu kuna mkataba fulani umeingiwa nadhani kuna mahala tunakosea,kwanini tunawapa gharama wananchi ambao wamezaliwa hapa kwenye rasilimali hii kwa mazingira ambayo tuliyatengeneza wenyewe tena makusudi ’’amesema waziri Biteko.

Pia waziri  Biteko amemwagiza afisa madini kupendekeza ni maeneo yapi yanayoweza kutolewa kwa  wananchi katika eneo mradi wa huo wa uchimbwaji wa chuma cha liganga na makaa ya mawe ya mchuchuma.

‘’Lazima tuvuke huo mstari inawezekana kweli kuna majadiliano yanaendelea lakini hayawezi kutufunga mikono na wananchi ambao wanahitaji kuchimba itakua wizara haina maana inachofanya,afisa madini nendeni mkapendekeze maeneo gani hata kama NDC tutamwambia kwamba uwezi kukaa na eneo hili lazima tugawe maeneo tuwakatie wachimbajiwadogo wachimbe na wakichimba uchumi wa hapa utakua’’alisema Biteko.

Waziri biteko ameongeza kuwa maamuzi kuzuia makaa ya mawe kutoka nje ya nchi lengo likiwa ni kuinua uchumi wananchi pamoja na wakazi wanaozunguka maeneo ya migodi kwa kuwa fursa za biashara zimehamia huko kutokana na juhudi zilizofanywa na serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema ujio wa Waziri Biteko mkoani Njombe ni wakati sahihi kwa kuwa wananchi na wachimbaji wadogo wanamatarajio makubwa ya kuona mkataba huu unafikia kikomo.

Mkoa wa Njombe mpaka sasa una leseni saba za uchimbaji wa madini huku 46 zinapendekezwa kufutwa.

No comments:

Post a Comment

Adbox