Wizara hiyo imesema watu hao wawili wametengwa huku wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Rafah.Matukio hayo yameongeza hofu ya kuzuka mripuko wa maambukizi hayo katika Ukanda Gaza eneo lenye wakazi wengi na huduma ya afya ambayo tayari imeelemewa.
Mamia ya wakazi wa Gaza wamerudi nyumbani katika wiki mbili zilizopita, lakini ni watu 92 pekee waliofanyiwa vipimo, hali inayoodhihirisha uwezo mdogo walionao wa kutoa huduma ya afya.
Gaza imetengwa mbali na ulimwengu tangu Israel na Misri zilipoiwekea vizuizi vya kusafiri baada ya kundi la Hamas kuchukua udhibiti wa eneo hilo mnamo mwaka 2007.


No comments:
Post a Comment