Adbox

Saturday, March 14, 2020

TAKUKURU yaokoa bilioni 8 ya vyama vya ushirika

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tanzania imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh8.8 bilioni katika vyama vya ushirika tangu Novemba 26, 2019 walipopewa kazi ya kuchunguza matumizi yake nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 14, 2020 jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema fedha hizo ni sehemu ya Sh124 bilioni walizoagizwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga kuchunguza.

“Uchunguzi unafanyika kwa awamu, awamu ya kwanza ilimalizika na taarifa yake ilitolewa Januari 22, 2020 na sasa tunatoa awamu ya pili na ya tatu itatolewa baadaye.”

“Mpaka leo tumeokoa Sh8.8 bilioni ambapo awamu ya kwanza tuliokoa Sh4 bilioni na awamu ya pili tumeokoa Sh4.8 bilioni,” amesema.

Amesema miongoni mwa Sh8 bilioni zilizookolewa wahusika wamezirejesha wenyewe na baadhi yao wamezirejesha baada ya mahojiano na Takukuru.

Kuhusu hatua zitakazochukuliwa, Mbungo amesema kinachofanyika sasa ni busara kuwaongoza kukusanya fedha kwani wakimweka mtu ndani siyo kupata fedha lakini baadaye wahusika wanaweza kupelekwa mahakamni.

No comments:

Post a Comment

Adbox