Mwanri ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa shughuli za Malipo kwa Ufanisi (RBF) kwenye Vituo na Zahanati mbali katika Wilaya ya Sikonge.
Alisema baada ya kumhoji Mhasibu wa Zahanati hiyo alimweleza kuwa Mganga huyo kupitia Dokezo alimtaka amlipe yeye kiasi cha fedha hizo ili akawalipe mafundi na vibarua walioshiriki kazi ambayo haionekani.
Mwanri alisema Mganga huyo asimame kupisha uchunguzi wa TAKUKURU kama itaonyesha kumefanyika wizi wa fedha za umma apelekwe Mahakamani na kama itaonyesha hakuna kosa basi aendelee na kazi yake.
Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa TAKUKURU wilayani Sikonge Magore Msena alisema walishapata taarifa za matumizi mabaya fedha za umma katika mradi huo wa kisima na walikuwa wakiendelea na uchunguzi na walikuwa mbio kuwachukulia hatua wahusika.
Alisema uchunguzi wa awali walibaini kuwa ni kiasi cha shilingi milioni mbili na sio milioni moja ndio kinaonekana kutumika katika kazi hiyo hewa .
Mkuu wa Mkoa wa Tabora akiwa wilayani Sikonge amefanikiwa kukagua Kituo cha Afya Mazinge, Zahanati ya Tutuo, Zahanati ya Pangale na Zahanati ya Usesula.


No comments:
Post a Comment