Adbox

Tuesday, March 3, 2020

Mbao, Yanga kuonyeshana ubabe leo

Leo michezo ya ligi kuu ya vodacom itaendelea ambapo timu ya Yanga itaonyeshana ubabe na Mbao FC mechi itakaypchezwa saa 1:00 usiku jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa leo Uwanja wa Taifa dhidi ya Mbao FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa ametumia muda mchache kuwaunganisha wachezaji wake ia wataifuata Mbao kwa tahadhari.

"Tumetoka kumalizana na Alliance hvyo unaona wazi kwamba ratiba imebana lakini imani yetu ni kuona kwamba tunapaya matokeo," amesema.

Mwezi Februari ndani ya ligi Yanga ililazimisha sare nne mfululizo ambapo ilianza mbele ya Mbeya City kwa kufngana bao 1-1, Prisons bila kufungana, Tanzania Polisi na Coastal Union.

No comments:

Post a Comment

Adbox