Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa Mradi wa reli ya Kisasa kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma, amesema kuwa kwakuwa mradi huu unazungumzwa katika vikao vyao ndio mana leo wamefanya ziara katika mradi huo.
"Leo tumekuja kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika eneo hili la mradi ambapo tunaona mradi unaenda vizuri kabisa."
Licha ya hivyo Reli ya kisasa itapita katika madaraja pamoja na Mahandaki ambayo yanaendelea kujengwa na Kampuni ya Yapi Markezi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa sekta ya Uchukuzi, katika Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamriho amesema kuwa kufikia Januari hadi mwishoni mwa Februari ni kiwango kizuri ujenzi utamalizika kwa wakati.
"Kufikia Mwezi Januari mwaka huu makandarasi walikuwa wameshafanya kazi kwa asilimia 25.8 hadi mwishoni mwa februari walikuwa wamefikia asilimia 28 kwa hiyo hicho kiwango ni kizuri tutamaliza kwa wakati."
Hata hivyo Makatibu wakuu na manaibu walitembelea mradi huo kwa kupita katika barabara inayotumika kujenga reli hiyo kuanzia jijini Dodoma hadi kufikia Mkoa wa Morogoro.


No comments:
Post a Comment