Tume ya taifa ya afya imesema maambukizi hayo yanawahusisha watu wanaowasili kutokea nchi za nje na yameripotiwa kwenye majimbo matano yakiwemo Beijing na Shanghai.
Kesi nyingine nne za maambukizi zimeripotiwa Wuhan mji mkuu wa jimbo la Hubei, ambako virusi hivyo vilianzia. Idadi ya watu waliofariki China kutokana na maradhi hayo imefikia watu 3,199 huku zaidi ya 80,000 elfu wakiambukizwa.
Jimbo la Hubei lilikuwa limefungwa mwezi Januari na kuwaweka karantini wakaazi karibu milioni 56, lakini idadi ya kesi mpya za maambukizi imepungua katika wiki za hivi karibuni.
Mamlaka za mji huo sasa zimeanza kulegeza baadhi ya hatua zilizokuwa zikiwazuia watu kutoka nje ya makaazi yao, ingawa hakuna dalili za watu kuondoka ndani ya jimbo hilo.

No comments:
Post a Comment