Kampuni hiyo imesema haitarejesha fedha badala yake abiria wote wenye tiketi katika safari zilizositishwa wanatakiwa kuwasiliana na ofisi za kampuni hiyo au wakala wa safari za ndege kwa ajili ya taratibu za kubadilisha tiketi hizo ili zitumike baadaye katika safari zao bila makato.
“Tumesitisha kwa sababu ya matamko na maagizo ya serikali mbalimbali katika nchi tunazofanya safari zetu, matamko hayo ni kufunga mipaka na kupunguza mwingiliano kwa sababu ya corona,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ACTL, Ladislaus Matindi.
“Tutarudisha safari hizo hali itakapoturuhusu. ATCL itaendelea kutoa huduma za ndani japo kwa kupunguza miruko katika baadhi ya vituo kutokana na upungufu wa abiria kipindi hiki cha tahadhali nyingi.”
Matindi ameahidi kampuni hiyo kuendelea kujali usalama na afya za wafanyakazi, abiria na wateja kwa kupuliza dawa, kusafisha kwa dawa maalumu ndani ya ndege na mikono.


No comments:
Post a Comment