Wakati huo huo, serikali ya Italia imesema inafikiria kuchukua hatua madhubuti kupambana na virusi vya Corona baada ya raia wake wawili kufariki kutokana na ugonjwa huo.
Kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 75 kilichoripotiwa jana karibu na mji wa Codogno huko Lombardy kimetokea siku moja baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 78 kufariki kutokana na virusi hivyo kwenye mkoa jirani wa Veneto.
Mripuko wa Corona nchini Italia, umesababisha huduma katika miji kadhaa kusimamishwa, huku kukiwa na ongezeko la wagonjwa 40 walioambukizwa.
Waziri Mkuu wa Italia, Giuseppe Conte ameelezea kusikitishwa na vifo hivyo na ameitisha mkutano wa dharura.


No comments:
Post a Comment