Tukio la kuzaa kwa wanyama aina ya Nyumbu limekuwa kivutio kikubwa kwa watalii waliofulika katika hifadhi ya Taifa Serengeti wakifuatilia maajabu ya mnyama aina ya Nyumbu anaye kubeba mimba na kuzaa kwa wakati mmoja, kusafiri umbali mrefu bila kuchoka akivuka mito na mabonde na baadaye kurejea bila kupotea alipotoka na kwamba anapozaa mtoto baada ya dakika saba mtoto huyo anauwezo wa kujihami na maadui.
Afisa uhifadhi ikolojia katika Hifadhi ya Taifa Serengeti Damari Nassary amebainisha tofauti wa Nyumbu walipo serengeti na maeneo mengine hapa duniani na kusema kwamba Nyumbu wenye maajabu mengi wanapatikana serengeti pekee hali inayowavutia watalii wengi kwenda kushuhudia maajabu mbalimbali ikiwemo kuzaa wanyama 500,000 katika kipindi cha wiki tatu.


No comments:
Post a Comment