Mwili huo uliosafirishwa kwa kutumia ndege ya kijeshi uliwasili na kufinikwa na bendera ya Kenya. Ulisindikizwa na msafara wa magari ya polisi , maafisa wa jeshi na familia ya Mzee Moi.
Helikopta ya kijeshi iliobeba mwili wa rais mstaafu Daniel Moi
Katika kaunti ya Nakuru ambayo ndio kaunti ya nyumbani kwa Moi waombolezaji walikaidi baridi ya asubuhi kutafuta maeneo watakayotazama mazishi hayo kwa kuweka milolongo mirefu katika uwanja wa chuo kikuu cha Kabarak siku ya Jumatano.
Maafisa wa usalama walionekana katika lango la chuo hicho mapema na walikuwa wakiwakagua waombeolezaji.
Raia walianza kuwasili katika uwanja huo mwendo wa saa kumi alfajiri . Baada ya kufanyiwa ukaguzi mkali wa kiusalama waombolezaji walipewa mkate na soda kabla ya kuingia.
Ukumbi wa ibada ya mwisho kabla ya kufanyika kwa maziko ya Moi
Kufikia mwendo was saa moja asubuhi , maelfu ya waombolezaji walikuwa wamemiminika katika uwanja wa chuo kikuu cha kabarak.
Tayari ibada ya mwisho imeanza. Moi atazikwa nyumbani kwake huko Kabarak baadaye hii leo katika maziko ya kitaifa ambayo yanafanywa na jeshi.


No comments:
Post a Comment