Adbox

Monday, February 17, 2020

Umoja wa Afrika wajipanga kukabiliana na virusi vya corona

Umoja wa Afrika unafanya kila linalowezekana kuhakikisha hatua madhubuti zinachukiliwa katika kukabiliana na mripuko wa maambukizi ya virusi vya corona katika bara hilo.

Taarifa hiyo ya asasi ya vituo vya udhibiti wa magonjwa barani, (Africa CDC), inafuatia uthitbitisho wa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa virusi hivyo vya Covid-19 kilichobainika Februari 14 nchini Misri.

Katika taarifa yake mkurugenzi wa Africa CDC John Nkangasong amesema wanataraji kwamba mripuko wa Covid-19 unaweza kuwa na athari kubwa kwa Afrika.

Katika jitihada za kuikinga Afrika na mripuko wa corona mkurugenzi huyo wa Africa CDC amesema taasisi yake umekuwa ikishirikiana bega kwa bega na mataifa ya Umoja wa Afrika katika kipindi cha wiki nne sasa kujipanaga katika utayari kukabiliana na matokeo yake.

No comments:

Post a Comment

Adbox