Katibu Mkuu wa zamani wa shirikisho la soka Afrika CAF Amr Fahmy ,36, amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa, Amr alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa CAF November 2017 kumrithi Hicham El Amrani lakini hakudumu hata kwa miaka miwili katika nafasi hiyo.
Amr mwaka jana kabla ya mauti yake alitangaza kuwa na nia ya kugombea Urais wa shirikisho la soka Afrika (CAF) ifikapo mwaka 2021, Amr aliondoka CAF katika nafasi ya ukatibu mkuu baada ya kushindwa kuelewana na Rais wa CAF Ahmad Ahmad.
Monday, February 24, 2020
Tanzia: Katibu Mkuu wa zamani wa CAF afariki dunia
Tags
# Top News
About Sultan Mapigo
SULTAN MAPIGO: Kuwa wa kwanza kuhabarika, Tafadhari usisahau kusubscribe kushare na kucomment
Top News
Tags:
Top News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment