Akizungumza mara baada yakukabidhi mifuko hiyo kwa viongozi wa kijiji hicho cha Mpwapwa, mwenyekiti wa TANECU, Shaibu Haifai Sadiki alisema msaada huo ni utekelezaji wa ahadi waliyotoa tarehe 21.12.2019 katika kijiji hicho wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo.
Alisema licha ya kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya nchini, lakini pia wao kama sehemu ya wadau wa maendeleo wameguswa na taabu wanazopata wananchi wà kijiji hicho kuhusu upatikanaji wà matibabu.
Sadiki alisema TANECU imekuwa ikichangia na kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kijamii katika sekta mbalimbali. Kwani inatambua kwamba wanufaika wa miradi hiyo ni wadau wake. Wakiwamo wanachama wa TANECU na wakulima wote.
Alisema ukosefu wa huduma za afya katika kijiji hicho unanafasi kubwa yakukwamisha shughuli za maendeleo. Kwani wananchi wanatumia na kupoteza muda mwingi wa kufanya kazi za maendeleo na kiuchumi kwa kufuta huduma hizo umbali mrefu.
" Kwahiyo tunaungana bega kwa bega na wakulima na wanachama wetu wanaoishi katika kijiji cha Mpwapwa, katika ujenzi wa zahanati hii. Walikuwa wanapata adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za matibabu," alisema Sadiki.
Kwaupande wake, mtendaji wa kijiji hicho, Ismail Ndivata alisema saruji hiyo itasaidia kuharakisha ujenzi wa zahanati hiyo ambao umefikia hatua ya linta. Huku akiweka wazi kwamba wananchi wa Mpwapwa wanapata huduma za afya katika kijiji cha Lengo, ambacho kipo umbali wa kilometa nane kutoka kijiji cha Mpwapwa.
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Harun Suleiman alisema jitihada za TANECU na wadau wengine katika ujenzi wa zahanati hiyo zinastahili kuungwa mkono na wadau wengine ambao wataguswa na kuhisi mateso wanayopata wananchi wa kijiji hicho kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.


No comments:
Post a Comment