Amesema kama Taasisi imeguswa na wahanga wa mafuriko mkoani Lindi hivyo kwani baadhi yao wamepoteza kila kitu hivyo japo wapate vitu hivyo.
Aidha amesema wataendelea kuwa pamoja na watanzania pale panapotokea majanga hayo.
Vitu walivyotolewa kwa wahanga wa mafuriko mkoani Lindi ni Nguo 600 Viatu Jozi 360, Unga Kilogram 2350, Vitabu 1250 pamoja na mashuka mazito 640.
Nae Meneja wa Kujiandaa na Kukabiliana na Majanga wa Tanzania Red Cross Jonston Weston amesema kuwa Wananchi wa Mkoa wa Lindi wanahitaji msaada kwani baadhi yao wamepoteza makazi.
Amesema kuwa katika elimu wanayoitoa kwa Wananchi ni pamoja kuwataka kufatilia taarifa za mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuchukua tahadhari mapema.


No comments:
Post a Comment