Adbox

Thursday, February 20, 2020

Mtayarishaji maarufu wa muziki nchini Marekani amuomba Daimondi wimbo wa gere

Mtayarishaji maarufu wa muziki nchini Marekani, Swizz Beats amemuomba msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz kumtumia wimbo wake mpya wa Gere.

Diamond ameuweka wimbo huo jana Jumatano Februari 19, 2020 katika mtandao wa Youtube na ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Katika Youtube, hadi saa 10:26 ulikuwa umetazamwa mara 425,178.

Beatz ambaye jina lake halisi ni Kasseem Dean aliandika ujumbe katika ukurasa wa Diamond wa Instagram, akimuomba amtumie wimbo huo, Diamond amekubaliana na ombi hilo.

Mtayarishaji huyo maarufu wa muziki ambaye ni mume wa msanii Alicia Keys ameshawatengenezea nyimbo wanamuziki maarufu  nchini Marekani akiwemo Beyonce katika wimbo wa Check on It na Ring the Alarm.

No comments:

Post a Comment

Adbox