Adbox

Monday, February 3, 2020

Mawaziri wa afya wa G7 kujadili kuhusu Corona

Mawaziri wa afya wa nchi zenye uwezo mkubwa wa kiviwanda duniani za kundi la G7 watajadiliana kuhusu virusi vipya vya Corona. Mkutano huo utafanyika kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa mujibu wa wizara ya afya ya Italia.

Idadi ya vifo kutokana na virusi hivyo nchini China imeongezeka hadi watu 361 kufikia jana Jumapili.

Mkutano huo wa G7 umepangwa kuanza mchana leo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo ya afya ya Italia ambapo mawaziri kutoka Marekani, Canada, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani Japan na Italia wataunganishwa kwa njia ya simu.

No comments:

Post a Comment

Adbox