“Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alipokua akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria aligusia suala la wapelelezi kuwa chanzo cha mlundikano wa mahabusu katika magereza yetu na mimi hii leo nimetoka gereza la Arusha nimeongea na wafungwa na mahabusu nao wanalalamikia upelelezi wa kesi zao kupindishwa na mbaya zaidi wengine wamehukumiwa vifungo kwa ajili ya upelelezi usio makini.Ni tatizo kubwa haiwezekani Rais huyu alalamike kila siku sasa maagizo ya serikali kwa chuo hiki jitahidini kupika vizuri wapelelezi wenu vizuri,tumpumzishe Rais wetu ana mambo mengi,timizeni tu wajibu wenu”amesema Masauni.
Akizungumza katika ziara hiyo Kaimu Kamandanti Kamishna Msaidizi Omar Khamis Omar amesema wamechukua maelekezo ya serikali na wanaahidi kuyafanyia kazi ili yaweze kuleta tija huku akitaja idadi ya wanafunzi waliopo shuleni hapo wakisomea fani mbalimbali.
“Shule yetu kwa sasa ina wanafunzi 856 kati yao wanaume 725 na wanawake ni 131 ambao wako katika mafunzo mbalimbali na wote wanaendelea vizuri na masomo” amesema Kamishna Msaidizi Omar
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Masauni alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo ikiwemo sehemu za kulala,madarasa,uwanja wa paredi,vyumba vya komputa na ukarabati bwalo la chakula.


No comments:
Post a Comment