Adbox

Tuesday, February 18, 2020

Mara: Wananchi waiomba serikali kuwarudishia eneo la malisho na kilimo Mlima Nkongore


Na Timothy Itembe Mara.

Wakazi wa mitaa ya Kwigoronto na Butirya Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara Taklibani  1200  wote kwa pamoja wameiomba Serikali kusikia kilio chao na kuwarudishia Eneo la malisho na kilimo,Mlima Nkongore lililochukuliwa hapo mwaka 2017 na kupewa Jeshi la Magereza kulitumia .

Mwenyekiti wa mtaa wa Butirya,Justine Maendeleo (56)akiongea kwa niaba ya wananchi wake juzi alisema kuwa maeneo ya kilimo na malisho ikiwemo shuguli za kuchota maji na kusenya kuni ya mlima Nkongore wamekuwa wakiyatumia tangu mababu zao lakini Mkuu wa wilaya aliyeondoka,Glorius Luoga aliyachukua na kuwapaJeshi la Magegeza kuyatuimia kwa madai kuwa maeneo hayo yalikuwa yakitumika kwa kilimo cha zao haramu la Bangi.

Maendeleo aliongeza kuwa uwamuzi wa mkuu wa wilaya aliyeondoka kuwapa Jeshi la Magereza naeneo hayo bila kiuwashirikisha haukuwafurahisha wananchi wa mitaa hiyo ambapo walianza kufuatilia kisheria ili kurudishiwa maeneo yao ili  kuanza kutumia kama ilivyokuwa tangu zamani lakini jitihada za kudai ziliendelea kugonga mwamba hadi hao wananchi pia wamechukua uwamuzi wa kwenda kwenye vyombo vya habari kutoa malalamiko na kuiomba serikali ya Awamu ya Tano kusikia kilio chao kwani hawana maeneo mengine ya mbadala ya kuendelea kutumia kwaajili ya uzalishaji mali pamoja na matumizi mengine ya kifamilia.

"Maeneo ya mlima Nkongore tumekuwa tukiyatumia tangu mababu zetu kwasababu ni uridhi tangu hapo kwa hali hiyo yametusaidia kwa shuguli za maendseleo kama vile kujenga kituo cha Afya Nkongore,Shule ya masingi Nkongore na shule ya msingi Ntaburu ambayo huwenda kwa sasa shule ya Ntaburo ikakwama kumalizika ujenzi kutokana na mguvu kazi kupungua baada ya  maeneo yetu tuliyokuwa tukiyatumia katika kilimo na kulisha mifogo  kuchukuliwa na jeshi la magereza na jamii kukoswa sehemu mbadala ya maeneo ya kutumia kwa ajili ya kilimo na uzalishaji mali"alisema Maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Kwigoronto,Charles Mgaya alisema kuwa kilio chao kwa serikali sikuvu ya Awamu  ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli nikuomba warudishiwe maeneo yao waliyokuwa wakiyatumia tangu mababu zao ili kuendelea kutumia kwa uhuru bila kubugudhiwa kama ilivyokuwa  tangu zamani na kuwa kilio hicho wanaomba kimfikie Rais ili warudishiwe eneo lao lililopewa Jeshi la magereza.

Kwa upande wake Samwel Matutu Mwita alisema kuwa maeneo hayo baada ya kuchukuliwa na mkuu wa wilaya aliyehama bila kuwashirikisha hapo 2018 na kuwamilikisha jeshi la magereza mwaka 2019 hawakuridhika badala yake walichukua hatua ya kulalamika kwanza kwa mkuu wa wilaya huyo ambapo waliandika barua ya tarehe 24,7,2018 na nyingine ya tarehe 5,4,2019 lakini malalamiko yao yaligonga mwamba baada ya mkuu wa wilaya huyo kuwaandikia barua yenye kumbukumbu namba AB.73/311/01D/127 ya Tarehe2,8,2018 .

Maombi ya kurudisha mlima Nkongore rejea barua yako ya tarehe 24,7,2018 katika barua hiyo umewsilisha umewasilisha maombi ya kurudishiwa mlima Nkongore pia umeambatanisha majina ya wananchi ambao umewatambulisha kama watumiajiwa mlima Nkongore wapo walioweka sahihi mahudhurio na ambao hawakuweka sainio baada ya kupitia barua yako napenda kukujulisha mabo yafuatayo,Mlima Ngongore wote ulikuwa ukitumika kwa kilimo cha zao haramu la Bangi kinyume cha sheria aliandika Luoga.

Luoga aliongeza kuwa wakati wote ambao kamati ya ulinzi na usalama imekwenda katika mlima Nkongore kuteketeza Bangi haijawahi kukutana na watumiaji wa mlima huo yaani wamiliki wa mashamba ya Bangi na mpaka sasa tunawatafuta pamoja na juhudi zote za kuteketeza mashamba hayo mara kwa mara bado kilimo cha Bangi kiliendelea tena kwa kasi zaidi serikali iliofanya maamuzi ya kutwaa eneo hilo na kuwaridhisha Jeshi la magereza ili kudhibiti kilimo cha Bangi ikumbukwe sheria inaelekeza kutaifisha mali na vyombo ambavyo vinatumika katika swala zima la madawa ya kulevya na kilimo cha madawa ya kulevya.

Flora Benard 58 alisema kuwa tangu aolewe alikuja akakuta wakwe zake wanamiliki maneneo ya mlima Nkongore na wanayatumia kwa shuguli za kifamilia na kama Jeshi la magereza linayachukua basi wapewe maeneo mengine makubwa kama hayo kwa shuguli zao,kama kigezo cha kuchukua maeneo yao ni kilimo cha Bangi basi maeneo mengi hapa nchini yalikuwa yakilima Bangi nayo yachukuliwe  na serikali na kama sivyo mkuu wa wilaya kuwapa mjeshi la magereza maeneo yao huo niuonevu wanaomba kilio chao kisikike.

Kwa upande wa Jeshi la magereza la wilaya Tarime,ASP,Deusdedit Yamo alisema kuwa maeneo hayo wamepewa kisheria na hawataki kuwa na mgogoro na wananchi wa maeneo hayo cha msingi kama wananchi hao hawajaridhia maeneo yao kuchukuliwa wadai kisheria ili kurudishiwa maeneo yao waliokuwa wakiyatumia siovinginevyo.

Mkuu wa wilaya Tarime mkoani Mara Mtemi Msafiri alisema kuwa eneo hilo wamepewa jeshi la Magereza kisheria na kama kuna malalamiko yeyote ambaye anamalalamiko ayapeleke Ofisini kwake vinginevyo maeneo hayo nimali ya magereza.

Msafiri aliongeza kuwa awali amewaelekeza wananchi hao kuachia maeneo hayo na kusitisha shuguli zote zinazoendelea kwa lengo la kuachia Jeshi la magereza ili kuendelea kufanya shuguli zake.

No comments:

Post a Comment

Adbox