Adbox

Sunday, February 23, 2020

Kenya: Jaji aliyedaiwa kushirikiana na mshukiwa wa mauaji kushtakiwa

Jaji mmoja nchini Kenya atafunguliwa mashtaka mahakamani kufuatia madai kwamba alishirikiana na mshukiwa wa mauaji.

Jaji wa mahakama ya rufaa Sankale Ole Kantai alikamatwa na maafisa wa jinai siku ya Ijumaa na kuhojiwa kuhusu uhusiano wake wa karibu na Sara Waimu , mshukiwa mkuu wa mauaji ya raia wa Uholanzi Tob Cohen.

Jaji huyo aliachiliwa siku ya Jumamosi mchana kwa dhamana baada ya kulala katika kituo cha polisi cha Muthaiga ambapo alikuwa anazuiliwa.

Mwili wa raia huyo tajiri kutoka Uholanzi ulipatikana katika shimo la maji taka nyumbani kwake jijini Nairobi 2019.

Maafisa wa polisi wanasema kwamba wana sababu za kuamini kwamba jaji Sankale alikuwa na uhusiano wa karibu na mshukiwa huyo ambaye amedaiwa kumpa ushauri ili kukabiliana na kesi yake mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Adbox