Adbox

Friday, February 7, 2020

Iran kutoa taarifa za shambulizi kwenye kambi ya Marekani

Iran imesema hivi karibuni itaweka wazi taarifa kuhusu shambulizi la kombora lililofanywa dhidi ya kambi ya Marekani nchini Iraq mwezi uliopita.

 Shirika la habari la Iran, ISNA limeripoti hayo leo, likimnukuu kamanda wa kikosi cha anga, Brigedia Jenerali Amirali Hajizadeh.

Mvutano umeongezeka kati ya Iran na Marekani baada ya kamanda wa ngazi ya juu wa kijeshi, Qassem Soleimani kuuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani kwa kutumia ndege isiyo na rubani Januari, 3 mwaka huu.

Mauaji hayo yaliichochea serikali ya Iran kulipa kisasi kwa kufanya shambulizi katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ain al Assad iliyoko nchini Iraq, siku chache baadae.

No comments:

Post a Comment

Adbox