Moi alifariki siku ya Jumanne wiki iliopita.
Mwili wake uliondolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee mapema alfajiri chini ya ulinzi mkali .
Wakenya walipanga milolongo mirefu ili kutoa heshima yao ya mwisho kwa rais mstaafu
Msafara wa jeneza lake ulienda hadi katika Ikulu ya rais.
watu katika uwanja wa nyayo
Msafara huo baadaye uliondoka katika ikulu ya rais na kuelekea hadi uwanja wa Nyayo mwendo was saa tatu asubuhi ambapo Wakenya walisubiri kuwasili kwa mwili wake kabla ya ibada hiyo.
Tayari baadhi ya viongozi waliowasili ni pamoja na rais wa Rwanda Paul Kagame, Salva kiir wa Sudan na rais Museveni wa Uganda
Kuanzia mapema ya saa kumi na moja alfajiri , watu walikuwa wamepanga milolongo mirefu kuingia katika uwanja huo.
Mabasi ya shule kutoka maeneo mbalimbali yaliotumika kubebba kusafirisha watu hadi katika uwanja huo , yaliegeshwa katika maeneo tofauti ya mji huku watu wakiwatakiwa kushuka na kupanga foleni karibu na barabara ya Bunyala.
Viongozi wengine waliowasili kwa ibada hiyi ya kitaifa ni marais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.
Mwili wake kwa sasa unazungushwa ndani ya uwanja huo polepole na kusindikizwana na wanajeshi kutoka jeshi la Kenya.


No comments:
Post a Comment