Meneja wa Maji RUWASA wilaya Rorya mkoani Mara,Emmanuel Masanja alisema katika baraza lamadiwani juzi kuwa halmashauri yake imepanga kukarabati na kufufua mradi wa maji Ochuna kata ya Nyathorogo ulioanzishwa enzi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati akiwa Rais mwaka 1986 na ukasahaulika na awamu tatu zilizopita ambapo umekuja kufufuliwa na awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli na watumiaji kunufaika.
Masanja aliongeza kuwa RUWASA wilaya Rorya imejipanga kutekeleza miradi 30 yenye jumla ya fedha 3,033,386,147.57 ambayoitahusisha ukamilishaji wa miradi mipya ya maji,ukarabati wa miradi ya bomba ya zamani na ujenzi wa miradi midogomidogo.
"Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Serikali ya India imepanga kutekeleza ujenzi wa mradi wa maji utakaotoa maji Ziwa Victorya (Kyangasaga)na kupeleka maji Tarime(miji ya Sirari na Tarime)vijiji 40 vya wilaya Rorya vitanufaika na mradi huo serikali ya Tanzania inasubiri kibali cha kutangaza zabuni ya ujenzi wa mradi kutoka serikali ya India"alisema Masanja.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya,Charles Chacha alisema kuwa katika mradi wa Ochuna uliosahaulika tangu awamu ya kwanza Enzi ya Mwal Nyerere na miradi mingine saba kukamilisha idadi ya miradi maji itakayo tekelezwa kuwa 8 kiasi cha shilingi 1,366,865,340 kimepokelewa.
Chacha alifafanua kuwa fedha hizo zitaenda kutekeleza miradi kwaajili ya ukarabati wa miradi 8 (miradi ya maji Ingirijuu,Marasibora/Nyanchabakenye,OchunaMasonga/Nyamagongo,Nyanduga,Sudi,Kowaki,Nyasoko na ujenzi wa miradi midogo midogo 2 kituo cha Afya Utegi na mradi wa mdogo wa maji Ng'ope).
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa hadi sasa kibali cha utekelezaji miradi hiyo kimeishatolewa,mchakato wa manunuzi wa vifaa(mabomba viungio wavu na pambu)unafanywa na RUWASA makao makuu na miradi itatekelezwa kwa Fouce Account baada ya vifaa kufika miradi inategemewa kukamilika ifikapo 30juni 2020.
Hezebon Danger alipongeza uongozi awamu ya Tano chini ya Rais wake John Pombe Magufuli katika utekelezaji wa miradi na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi kwa maendeleo ya wananchi hususani katika kufufua mradi wa maji Ochuna.
Danger aliongeza kuwa mradi wa maji Ochuna ulianzishwa na Rais Julius Kambarage Nyerere wakati akiwa anasoma shule ya msingi hapo mwaka 1967 na mradi huo ukafa kwa kuhujumiwa na wakora wasiojulikana na kama utafufuliwa na kuanza kazi wananchi wengi watanufaika na mradi huo badala ya kutaabika.
Mwananchi huyo aliongeza kuwa mradi wa maji Ochuna ni kati ya miradi miwili ya maji mkoami Mara iliyoanzishwa na mwalimu Nyerere mwaka 1967 moja ukiwa huo wa Ochuna na mwingine ukiwa wilaya Butiama kwasababu tu wilwyw hizo zilikuwa zinakubwa na ukame mkubwa ikilinganishwa na wilaya zingine za mkoa Mara.


No comments:
Post a Comment