Ameongeza kuwa kwa ufadhili wa UNDP, ESRF ikishirikiana na Serikali za Mikoa limefanya utafiti kuainisha fursa mbalimbali za uwekezaji katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na mpaka sasa imekwisha kamilisha kutayarisha Miongozo ya Uwekezaji wa Mikoa 15 na inaendelea kumalizia mikoa mingine iliyobaki. Amesema katika miongozo hiyo fursa nyingi zinatoka katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
Bi Nzuki amewaambia washikiri kuwa lengo la Kongamamo hilo ni kushirikishana na kutoa maarifa mapya katika kilimo biashara
Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kukua kwa teknolojia duniani kumeongeza fursa nyingi na kuwezesha wakulima katika sehemu mbalimbali duniani kutokutegemea mvua.
"Teknolojia imewezesha wakulima kutumia eneo dogo la ardhi kuzalisha kiwango kikubwa cha mavuno ya mazao yaliyo bora; teknolojia pia imewezesha wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo cha kisasa toka kwa wataalamu kwa haraka na muda muafaka, hivyo kusaidia kupata mavuno mengi na bora," alisema Dk. Kida.
Kilimo hicho cha kutegemea teknolojia za kisasa kinachoitwa kwa kiingereza “Smart Farming Agriculture” ambacho hakihitaji maeneo makubwa ya ardhi na kinaweza pia kufanyika katika miji.
Uwingi na ubora wa mazao yanayozalishwa ni kiashiria cha fursa ya kufanya biashara kwa tija, kwa sababu mazao hayo yatamvutia mnunuzi na yanaweza kuuzwa popote duniani kutokana na sifa zake za ubora; mfano kwenye maduka makubwa na mahotelini ambako wateja wengi katika zama hizi wanapenda vyakula vya asili ambavyo havina kemikali ambayo inatumika kukuzia mimea mashambani.
Kongamano hilo limeandaliwa kwa ajili ya wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine katika sekta ya Kilimo.
kwa mujibu wa Dk. Kida wakufunzi mbalimbali waliobobea na wanaojihusisha katika fani mbalimbali za Kilimo biashara wametarajiwa kutoa uwelewa kwa kuwajengea uwezo washiriki ili kutafuta utatuzi wa vikwazo mbalimbali ambavyo wakulima na wafugaji mmekuwa mnakabiliana navyo.
Katika kongamano hilo lililofanyika mwishoni mwa juma mada zilizofundishwa naa kujadiliwa Kwa kina ni pamoja na:malisho ya chakula cha samaki,ufugaji wa samaki katika matanki (Recirculating Aquaculture System), kilimo cha mboga mboga bila kutumia udongo (Hydroponic Vegetable),kilimo cha azolla kwa ajili ya malisho ya mifugo na mbolea, ufugaji wa kisasa wa samaki kwa kutumia vizimba, matanki na mabwawa,ufugaji wa kisasa wa nyuki na kubadilishana uzoefu katika kilimo biashara.
Washiriki wengine pamoja na wakulima na wafugaji ni taasisi za fedha nchini za TADB, CRDB, SELF na PASS Trust.
Wadau hao hutumiwa na wadau wengi katika kufanikisha mipango ya maendeleo kwa manufaa ya mtu mojammoja, vikundi na Taifa kwa ujumla.

No comments:
Post a Comment