DC Katambi ameitoa kauli hiyo wakati wa uwasilishaji wa mpango na bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka fedha 2020/21 uliotolewa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Katika uwasilishaji wa mpango na bajeti hiyo, TARURA Dodoma Jiji imesema imepanga kukarabati na kutengeneza kilomita 332.20 na vivuko sita kwa gharama ya Sh Bilioni Nne.
Akizungumza katika baraza hilo DC Katambi amesema uwepo wa taasisi hizo ikiwemo TARURA kwenye baraza la madiwani kutawasaidia kujua changamoto zilizopo kwani madiwani ndio wenye kujua kero na matamanio ya wananchi.
" Taasisi zote zilizopo kwenye Jiji la Dodoma iwe Tanesco, TARURA, DUWASA tuhudhurie vikao hivi kwa sababu kwenye maeneo ambayo tunasema tuna changamoto za kibajeti hatuwezi kufika Mbabala, Kikombo au Zuzu hawa madiwani ndio wanatoka hayo maeneo na wanajua vizuri kero zilizopo kuliko sisi tunaoenda mara moja.
Hivyo ni muhimu sana kuwepo kwenye mabaraza. Na hivyo nimtake Katibu Tawala wetu wa Wilaya kuziandikia taasisi zote barua kwamba katika vikao vyote vya madiwani wafike na wasikie changamoto na ikiwezekana wajibu changamoto zote zinatolewa hapa," Amesema DC Katambi.
Amesema kwa kufanya hivyo kumtarahisishia kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuepuka lawama z wananchi kwani taasisi hizo zikijua changamoto zilizopo kwenye maeneo ya Jiji itakua rahisi kwao kuzitatua ili wananchi waone namna ambavyo serikali yao inatatua shida zao.


No comments:
Post a Comment