Kajale alisema kuwa wataalamu hao wameajiliwa na Ushirika huo kwa ajili ya kuwapatia elimu ya namna ya kuendeleza kilimo cha kisasa, ili kupata mavuno ya uhakika kama ilivyo dhamira yao kwenye mashamba ya Ruvu yaliyopo Kitongoji cha CHAURU Kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza.
"Wakulima wa CHAURU niwaombe tuwatumie wataalamu ambao tumewaajili kwa lengo ya kupata elimu ya kilimo cha kisasa, hatimae kupata mavuno ya uhakika kama dhamira yetu ya ushirika wetu," alisema Kajale.
Mary Ngauga aliutaka uongozi kuwajulisha mali na majengo ya ushirika huku akigusia mchanganuo wa mapato yaliyokuwemo kwenye taarifa iliyoandaliwa na uongozi wao chini ya Mwenyekiti wao Sadala Chacha.
Kwa upande wake Dkt. Msuya alitaka kujua ukaguzi wa kimahesabu za chama kupitia COASCO, huku akitaka kufahamu ukaguzi wa ngapi, kwani ameshangaa kuona kama ndii ukaguzi wa kwanza wakati ushirika huo ni wa muda mrefu.
Akitolea ufafanuzi wa maswali hayo, sanjali na mapato ya chama, Chacha alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 400 zilizooneka kwenye taarifa sio zao na kuwa wao ni mawakala tu, huku akifafanua kuwa ushirika unanufaika na fedha zitokanazo na kinu cha kukobole mpunga.
"Kwa mwaka huu tumeshapeleka barua ya kuomba tuwe tunalipia kodi TRA, tumeambiwa tuje tufanye mahesabu ya mapato yetu tunayokusanya ili utaratibu mwingine fuate," alisema Chacha.
Aliongeza kuwa miaka iliyopita wajumbe wa bodi ndio walikuwa watendaji, ndio maana mwaka huu wameajili wataalamu wenye taaluma, huku akigusia hati za mashaka walizokuwa wanazipata zilitokana na kutokuwepo kwa wataalamu hao.
Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa muda Moses Polepole, wana-CHAURU hao wamekubaliana kulipa madeni yao ndani ya chama ifikapo mwisho wa mwezi wa tisa, muda ambao wanachama wote watakuwa wameshavuna.


No comments:
Post a Comment