Adbox

Friday, February 7, 2020

Bei za Bidhaa zimeongezeka kwa asilimia 4.9

Na Thabit Madai,Zanzibar.


Kasi ya mfumko wa bei za bidhaa imeongezeka kufikia asilimia 4.9  kwa mwaka 2020 ukilinganisha  na asilimia 3.3  kwa mwaka 2019.

Hayo ameyasema Mkuu wa Kitengo cha mfumko wa bei kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali  Khamis Abrahmani Msham wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mtakwimu Mkuu wa Serikali ilioko Mazizini.

Amesema vyakula vilivyoongezeka bei ni pamoja na Mchele wa Mbeya 1.8 Unga wa Sembe 46.2 , Unga wa Ngano 2.5, Samaki 6.9, Ndizi Mbichi 14.8 Sukari Nyeupe 5.5 Ndizi mbivu 5.4 na Saruji 1.2.

Pia amesema kwa mwezi wa January 2020 bei imeongezeka kwa asilimia 1.2 ikilinganishwa  na 0.8 kwa mwezi wa Disemba 2019.

Nae Mhadhiri wa Uchumi Zanzibar Suleiman Simai Msaraka amesema sababu kubwa iliyosababisha kupanda chakula kutokana na mabadiliko ya  hali ya hewa ikiwemo upepo  mkubwa.

Amesema Serikali itashughulikia suala la upandaji wa bei ya chakula na pia kwa upande wa Kenya haijatufikia bei iko juu zaidi kuliko Zanzibar.

Kwa upande wake Afisa Uchumi wa Masoko wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na  Maji ZURA Omar Ali Yussuf  amesema kwa upande wa mafuta  bei haiko kubwa.

Alisema kwa kipindi hiki hali ya mafuta iko vizuri kutokana na utulivu wa  Soko la Dunia.

Nao wananchi wamesema hivi sasa hali ya bei imezidi kuwa kubwa hali ambayo inawasababishia kutoweza kumudu kupata mahitaji ya lazima ikiwemo samaki, nyama   bidhaa za nafaka, na baadhi ya bidhaa nyengine.

No comments:

Post a Comment

Adbox