Adbox

Sunday, December 8, 2019

Wakuu wa Wilaya Songwe wametakiwa kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza

Na Baraka Messa, Songwe

Serikali mkoani Songwe imewataka wakuu wa Wilaya wakishirikiana na wakurugenzi watendaji kuhakikisha wanakamilisha miundo mbinu ya madarasa ili wanafunzi 15,076 waliofaulu katika matokeo ya darasa la saba kwa msimu wa mwaka 2019 wote kuanza kidato cha kwanza pindi shule zitakapofunguliwa mwezi january 2020.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe David Kafulila akimwakilisha mkuu wa mkoa katika kikao cha taarifa ya Matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2019 na uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2020 alisema wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhakikisha wanatatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtoto aliyefaulu anajiunga na kidato cha kwanza ifikapo januar 2020 shule zinapofungua.

Kafulila aliwasisitiza viongozi hao wa halmashauri kufanya kila linalowezekana kukamilisha miundo mbinu ya madarasa, vyoo na madawati ambavyo vimekuwa vikichangia miaka mingi ya nyuma watototo kuchelewa kuanza masomo na kupelekea kiwango cha ufaulu kuwa kibaya.

"Ifikapo januari shule zinapofungua hatutaki kuona mtoto yeyote anabaki nyumbani kusubiri kukamilika kwa madarasa, mpaka hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa halmashauri ya Momba upungufu ni vyumba vya madarasa 16 ambavyo inatakiwa kukamilika kabla ya januri ,Halmashauri ya Ileje vyumba 7,Halmashauri ya Tunduma 49, Halmashauri ya Songwe vyumba 9 na Halmashauri ya Mbozi vyumba 65" alisema

Aidha Katibu tawala kafulila amesema usimamizi wa elimu kwa mkoa wa Songwe bado sio mzuri jambo lilopelekea matokeo ya darasa la saba kwa msimu wa 2019 kuporomoka  kutoka nafasi ya 17 mpaka nafasi ya 21 kati ya mikoa 26 kitaifa.

"Kwenye usimamizi wa elimu maafisa elimu kata na Tarafa bado hawajafanya kazi yao kuna walimu watolo na wanafunzi watoro lakini walimu wakuu na wasimamizi wa elimu wamekaa tu wanaangalia, hatutawavumilia walimu wakuu  na wasimamizi wa elimu hivi sasa watakaoshindwa kufanya majukumu yao na kupelekea matokeo kuporomoka kitaifa " aliongeza kafulila.

Kwa upande wake afisa elimu mkoa wa Songwe Juma Kaponda alisema matokeo ya darasa la saba msimu wa 2019 kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa kiasi kikubwa kutokana na udhaifi wa wasimamizi wa elimu katika ngazi ya walimu wakuu na maafisa elimu kata.

Alisema Takwimu zinaonyesha kuwa kwa matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2017 mkoa wa Songwe ulikuwa na wastani wa asilimia 63 ukishika nafasi ya 23 kati ya mikoa 26 nchini, mwaka 2018 mkoa ulikuwa na wastani wa ufaulu wa asilimia 74 ukishika nafas ya 17  na mwaka huu 2019 mkoa umeshika nafasi ya 21 ukiwa na wastani wa 75.5 ukishika nafasi ya 21 kitaifa.

"Tumebaini kuwa pia ripoti za ukaguzi hazifanyiwi katika shule zetu hazifanyiwi kazi baada ya kukaguliwa, wakurugenzi watendaji wa Halmashauri someni na kuzifanyia kazi ripoti zinazotolewa na wakaguzi wetu ili kuboresha mapungufu yaliyopo katika shule zetu za Msingi na Sekondari " alisema Kaponda.

Ubatizo Songa mwenyekiti wa halmashauri ya Ileje alisema kuwa uhaba wa walimu katika Halmashauri yake unachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha ufaulu ambapo kuna baadhi ya shule mwalimu mmoja hulazimika kufundisha madarasa manne.

No comments:

Post a Comment

Adbox