Adbox

Sunday, December 8, 2019

TANZIA: Mfanyabiashara mashuhuri Tanzania Ali Mufuruki aaga dunia

Mfanyabiashara mashuhuri nchini Tanzania Ali Mufuruki amefariki dunia leo nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mufuruki ambaye ni muasisi wa Jukwaa la Maofisa Watendaji Wakuu – CEO Roundtable na mmiliki wa kampuni ya Infotech Investment Group Limited na maduka ya Woolworth alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu mjini Johannesburg.

Mwenyekiti wa CEO Roundtable Sanjay Roughani amethibitisha kifo hicho akisema kuwa Mufuruki alianza kuugua akiwa Dar es Salaam na akapelekwa katika hospitali ya Agha Khan na kisha akapelekwa Afrika Kusini jana mchana.

Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na miaka 60 aliwahi kuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom Tanzania na Wananchi Group Holdings.

No comments:

Post a Comment

Adbox